12 Julai 2025 - 13:14
Source: ABNA
Maandamano nchini Mauritania Yakilaani Uhalifu wa Utawala wa Kizayuni

Maelfu ya Wamauritania wamefanya maandamano kupinga mauaji ya halaiki yanayofanywa na Wazayuni katika Ukanda wa Gaza na pia kutangaza kuunga mkono upinzani wa Palestina.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (ABNA), maelfu ya raia wa Mauritania walifanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo kulaani mauaji ya halaiki yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.

Maandamano hayo, yaliyokuwa na kauli mbiu "Gaza: Upinzani na Ustahimilivu," yalianzia mbele ya Msikiti Mkuu wa Nouakchott na kuendelea hadi Ofisi ya Uwakilishi wa Umoja wa Mataifa.

Waandamanaji walibeba bendera za Mauritania na Palestina, pamoja na picha za viongozi wa upinzani wa Palestina, wakiwemo mashahidi Ismail Haniyeh na Yahya Sinwar, wakipiga nara za kuunga mkono upinzani wa Gaza na kulaani uhalifu wa utawala wa Kizayuni unaokalia kwa mabavu.

Mkutano huu uliitishwa na mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali na unachukuliwa kuwa sehemu ya mfululizo wa programu za wananchi kuunga mkono taifa la Palestina.

Washiriki wa maandamano haya waliilaumu moja kwa moja Marekani kwa kuendeleza vita na mauaji ya halaiki huko Gaza.

Your Comment

You are replying to: .
captcha